google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 19, 2018

Ukifuata Ushauri Huu, Kamwe Mafanikio Hayatakusumbua.

No comments :
Haijalishi unapitia changamoto za kiasi gani, haijalishi maisha yako ni magumu kiasi gani, ipo njia ya kuweza kukutoa hapo na kukufanya ukawa na maisha bora ikiwa utaamua kuifanyia kazi kwenye maisha yako.
Sizungumzii habari za ndoto, nakwambia njia ambazo zinafanya kazi na kuleta mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako. Hakuna muujiza wala uchawi ni swala la kufata kanuni na kutekeleza, hutaki sahau mafanikio kwani huwezi kuyapata.

1. Jitoe kwenye ndoto zako.
Weka kila kinachohitajika ili kutimiza ndoto zako. Weka nguvu na juhudi, weka maarifa, yaani kwa kifupi fanya kila linalowezekana kuhakikisha ndoto zako zinatumia. Ikiwezekana tumia kila aina ya maarifa yaliyo muhimu yakusaidie kukupa mafanikio yako ambayo unayataka. Ukijitoa ni uhakika kufanikiwa.
2. Tafuta maarifa.
Kujitoa ni muhimu sana kwako ili kuweza kufanikiwa. Kujitoa huko hakuwezi kukufikisha mbali kama bado hutafuti maarifa ya kuweza kukusaidia katika hicho unachokifanya. Kuna makosa mengi sana ambayo utakuwa unayakwepa kama wewe utakuwa ni mtu wa kutafuta maarifa. Maarifa ukichanganya na kujitoa kwako, utafika mbali.
3. Fanya kazi sana.
Uwe maskini wa kutupwa unalala chini ya daraja au uwe unalala mtaani au kwa vyovyote vile. Ukichagua kufanya kazi hapo hakuna tena atakayekuzuai kufanikiwa, fanya kazi usiku na mchana. Usikubali kukaa katika mkono mlegevu wakati unahitaji mafanikio ya kweli. Fanya kazi ikusaidie kukufikisha kwenye ngazi ya mafanikio makubwa.
4. Vumulia na usikate tamaa mapema.
Mafanikio yanakuja kwa watu wote ambao wanavumulia na hawakati tamaa mapema, nawe pia unatakiwa uwe miongoni mwao. Najua unakutana na mambo mengi sana lakini vumilia kila hali na usiruhusu kukata tamaa hata kidogo. Ukiweza kuvumilia na kuacha kukata tamaa mapema utafika mbali sana kimafanikio.
Fanyia kazi mambo haya na uwe na uhakika mafanikio kwako hayataweza kukusumbua kwa kitu chochote kile kwako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.