google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 20, 2018

Utatengeza Mafanikio Sana Kama Utaacha Kitu Hiki.

No comments :
Thamani unayoitengeneza kwenye maisha yako, haitegemei sana na wingi wa vitu unavyovifanya kwenye maisha yako, bali thamani hiyo inategemea zaidi ni jinsi gani unaweka nguvu zako nyingi kwa vitu vichache lakini vikaleta matokeo.
Kwa siku unaweza ukawa unafanya mambo mengi sana, kwa mfano unagusa hili, kabla hili haijaisha unataka uguse lile, sasa kufanya mambo haya kwa wingi na kwa namna hii hakuwezi sana kukusaidia.
Unatakiwa nguvu zako nyingi sana uziweke sehemu moja, uziweke sehemu ambayo itakupa matokeo. Hata kama una juhudi vipi, kama nguvu zako nyingi unazitapanya kwa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ni ngumu sana kuweza kufanikiwa.
Inatakiwa umakini, unatakiwa kuelewa wakati huu unafanya nini, na hivyo mawazo yako yote unatakiwa kuyahamishia eneo hilo mara moja na si kutanga tanga kwa kujaribu kugusa kila kitu, huwezi kufanikiwa kwa namna hiyo hata siku moja.
Thamani unayotoa na inategemea sana pia na muda unaoutumia katika kufanya jambo hilo. Unatakiwa kutumia muda mchache kufanya makubwa. Utajitengenezea sana mafanikio kama wewe utaacha kutanga tanga na mawazo yako huku na kule.
Utulivu katika kutafuta mafanikio yaani kuweka mawazo yako kwenye kitu kimojja ni jambo ambalo linahitajiwa sana. Kwa sasa naweza kusema watu wengi hawana utuliviu kabisa, wanarukia hiki au kile ili mradi tu.
Kama nilivyosema nikwambie hivi, utatengeneza sana mafanikio, kama utaamua kufanya mambo machache na kwa utulivu na ya kakupa mafanikio na sio kuruka ruka tu, kama ambavyo unafanya.
Zingatia haya machache na uwe na wakati mwema wa mafanikio kwako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.