google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 12, 2018

Usiache Siku Yako Ikaisha Bila Kufanya Mambo Haya.

No comments :
Yambo mambo matatu ambayo hutakiwi kuacha kuyafanya kila siku. Kwa kifupi, kila siku inapoanza na hadi inapoisha ni lazima uhakikishe mambo hayo umeyafanya kikamilifu. Mambo hayo yatakusaidia sana kukujenga kwenye maisha yako kwa jinsi siku zinavyokwenda mbele.
Mambo haya muhimu ambayo nataka wewe rafiki yangu uyajue ni kama haya yafuatayo;-

1. Kujifunza.
Ni muhimu sana kuhakikisha umejifunza kitu cha kukusaidia kwenye maisha yako kila siku, akili yako lazima iweke kitu. Usiache siku yako ikaisha hivi hivi tu, weka kitu cha kukusaidia akilini mwako.
Kila unapoamka jifunze kitu, na endelea kujifunza kwa siku nzima. Ukijfunza inakusaidia sana kukukomaza kifikra na kukujengea akili ya mafanikio maishani mwako kila wakati. Watu wanaojifunza na kufanyia kazi ndio wanaofanikiwa pia kwenye maisha.
2. Kutoa upendo.
Ni muhimu pia sana kwako kutoa upendo ulionao na kwa wengine pia kila iitwapo leo. Hutakiwi kuishi kwa uadui, upendo unahitajika ili kuifanya dunia iwe sehemu salama kwako na kwa wengine pia.
Kama una ugomvi na watu achana na watu hao. Ishi maisha ya upendo kwa kuwapenda wengine na hiyo itakusaidia kujenga mahusiaono mazuri sana ambayo yataweza kudumu kwa muda mrefu na kwa manufaa.
3. Kutoa kila ulichonacho kikamilifu.
Huhitaji hapa kuuliza, ni lazima utoe kila ulichonacho kwa ukamilifu wote kupitia kazi unayoifanya. Nini unafanya hapo ulipo, toa uwezo wako woote yaani usibakishe kitu kama ni juhudi weka zote.
Kama ni maarifa ya aina fulani uliyonayo, hakikisha pia unatoa yote kwa ukamilifu ili kuwasaidia wengine. Kwa kila ukifanyacho, kitoe kwa ukamilifu sana ili kiweze kuleta msaada na matokeo bora kwa watu wengine kwenye maisha yao pia.
Ukifanyia kazi mambo hayo yatakusaidia sana kuweza kupiga hatua na hata kubadilisha maisha yako.
Uwe na wakati mwema na siku njema pia, kila la kheri na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kuweza kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.